Inasikitisha sana sana, na nimeshindwa kuvumilia........

blogger templates

Jamani kwanza natanguliza shukrani zangu za dhati, na nawaomba msamahaa wadau wangu wote, kwa kuwa this week nimelega lega ku upload blog hii yangu.

Mimi ni muajiriwa kwenye N G O moja hivi jina kapuni as a secretary/admin. Sasa kuna nafasi za kazi zimetangazwa na watu wame apply, kwa njia ya email na P. O. Box.

Njia ya email wangine hawa ja attach hizo documents, wengine wametuma tu CV etc. kama mtu huwezi kutumia email sio lazima tumia postal address na kwa Dar kwa Dar inawahi kufika.

Nimekuwa nikifungua hizo barua zao, lol nyingi ni vichekesho kwa kweli, na utakuta mtu ana degree, masters etc.

Najua sio kazi yangu na pia sio lengo la hii blogsite kwa yote hayo ila nimeguswa sana sana, kwani Barua ni utambulisho tuu na haitakiwi kuwa na mambo meengi mpaka employer akachoka kusoma. CV ndio ya kukuelezea wewe na ndio unajiuza kwa huyo new employer.

Kulikuwa na blogsite mpya ya kueleza jinsi ya kuandika barua za kuomba kazi, cv etc. ila naona siku hizi haja update muda mrefu sijui ni vipi.

Nawaomba wadau wangu tuingie katika hii mada tusaidiane kwenye mada hii mtuonyeshe jinsi ya kuandika barua za kuomba kazi na cv.

Tusaidiane kwa hili jamani, mimi nitakuwa ni mtu wa mwisho kuonyesha jinsi barua na CV zinavyotakiwa kuandikwa just Format.

0 Response to "Inasikitisha sana sana, na nimeshindwa kuvumilia........"

Posting Komentar