WOMENS CELEBRATION...MARCH 3 - TO ALL THE SINGLE MOTHERS OUT THERE......

blogger templates
Napenda kuwajulisha kua, kwa wale wote watakao penda kujumuika nasi katika siku hii, kuna mabadiliko kidogo, niliongea na Shamim, muandaaji wa event hii na akashauri tuchukue meza, ambayo ina viti kumi, na kila kiti ni 50,000/- so kama ni viti 10 ni shs. 500,000/.

Najua kua kwetu sie hii hela ni nyingi ila tukianza kujikusanya mapema hii itapatikana, na tutakaa meza moja, ama meza zitakazopatikana kutokana na wingi wetu, na siku hii basi, ndio itakua ni siku ya kujuana, na tutapanga ni siku gani tukutane ili tujue tunasaidianaje, na tunafanyaje. kujiendeleza.

Mimi aim yangu ni kwamba, tusaidiane, na ifike siku moja tuwe tunaheshimike, kunamsemo unasema UKIONA MWENZIO ANANYOLEWA, NAWE TIA MAJI ......

Jamani, inawezekana kabisa, tukiamua, na kukubali hali zetu....... tusisikilize nani anasema nini, angalia nafsi yako nini inataka, na unataka mtoto wako akue katika mwenendo gani. Ninaamini kabisa kwa kufanya hivi, tutafika mbali, na kupunguza mambo ya ajabu na kuchezeana......

Sisi,  tutakua ni waanzilishi tuuu, ila tukikutana tutachagua viongozi, mwendesha blog etc, nataka tugawane nafasi, na kusaidiana.

SINGLE MOTHERS TUNAWEZA, NA TUTAWEZA.......LOVE YOU ALL......

NB: NAKARIBISHA USHAURI KATIKA HILI,,,,siku zimekwenda.....   kwa atakaependa kujumuika nasi, pls tuwasiliane, ili tupeleke hela kwa pamoja tupate meza yetu.......

TUTANOGAJE SIKU HIYO.........THEME NI KHANGA, AND WE HAVE TO DRESS AND LOOK SEXY..........

0 Response to "WOMENS CELEBRATION...MARCH 3 - TO ALL THE SINGLE MOTHERS OUT THERE......"

Posting Komentar