JAYDAN HAS REACH 1 YEAR TODAY 8/2/2012. Happy Birthday my son.....I love you.....Mungu akubariki na kukuepushia mabaya.....

blogger templates



Hi all, napenda kumshukuru mungu kwa kila jambo analonitendea, mimi na jaydan, kwa kweli sintotaka kua muongo, nimepitia katika, mabonde, milima, etc.... Lakini mungu yuko nami mpaka sasa na anaendelea kua nami.


Nawashukuru pia wadau wangu kwa kua nami katika kipindi hiki chote, cha mpaka mtoto wangu Jaydan amefikisha mwaka 1, kwani mmenivumilia, na kuniamini na kunipa kazi zenu, na ninazifanya kwa usahihi mkubwa.

Nakumbuka nilivyokua mjamzito, nilitoa picha yangu, hapa kwenye blog, kuna mdau ali comment kua, sylvia usidhani ni rahisi kua single mum..... baadae nilijiuliza, bila majibu, ila kadri siku zinavyozidi kwenda, nilikuja kuelewa nini alimaanisha,..

Kweli kua single mum, ni kazi, ila nimejifunza mengi, kupitia mtoto wangu, kwani kwanza ninafanya kazi kwa bidii nikijua kua nina mtoto ananitegemea, mtoto wangu ndio faraja yangu hapa duniani, emagine ninarudi nyumbani nimechoka, jayd wangu ananipokea, nina hasira zangu, jay ananichekea, yaani ni raha kweli.....HALAFU KITU KINGINE, JAYDAN WANGU NDIE ATAKAEKUA LOVE TEST WANGU, KWANI AKITOKEA MTU ANANIPENDA, KWANZA NTAMWANGALIA KAMA ATAMPENDA MTOTO WANGU, NA SI UNAJUA KUNA YALE MAPENZI YA KUJIFANYISHA, NTAMBALASA... NA KAMWE SITAMUACHA MTOTO WANGU KWA MTU, KOKOTE NIKO NAE ETI SIO KESHO NAOLEWA NAMUACHA MWANANGU KWA MTU........PATACHIMBIKA....etc..

Leo Jaydan amefikisha mwaka 1, nina furaha isiyo kifani, kwanza kua mama, na pili ninajitahidi ku balance muda wa kazi na mtoto. ninaanza ku save hela ya shule yake,.... jamani ukijipanga hata mungu anakuona na atakusaidia, nakuhakikishia huto oomba hela kwa mtu, unajikuta tuuu maisha yanakwenda smooth...

Sasa basi napenda kuwahusia single mothers wote, kua wasilalamike, wala kunung'unika, kwani mungu ndie mpangaji wa yote. Hebu jiulize ni wanawake wangapi mpka leo wanatafuta watoto, na hawajapata, ila wewe mungu amekubariki na umepata mtoto? Na haujapata mtoto na wote uliokua nao ukapata mtoto na huyo uliezaa nae? Na ujue wewe si mgumba....MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO.....

Mimi niliweka mikakati na ambayo inanisaidia sana mpaka sasa, nimepunguza matumizi yasiyo na maana, nilikubali kujishusha, ninasikiliza ushauri, ninajishughulisha na kazi zangu yaani sina muda wa kufikiria mwenzangu anafanya nini na yuko wapi.......ama kwenda kumfanyia fujo....huo muda sina kabisaaaa,


Nawashukuru wale wote walio kua karibu nami katika kipindi hichi chote, na bado wako nami,,,Halima, Phides,Sylvia,Jossyanne,Nuru the Light, Dina, na familia yangu.

Jua kua wewe ni single mother, unaweza na utaweza, wewe ni mzuri, kubali kua uko peke yako, na mtoto ni wako....... na muombe sana mungu akutangulie katika kila jambo.........it's hard but you can make it without him .....hongereni kwa kua na watoto........ Nawapenda wooteeee

0 Response to "JAYDAN HAS REACH 1 YEAR TODAY 8/2/2012. Happy Birthday my son.....I love you.....Mungu akubariki na kukuepushia mabaya....."

Posting Komentar