Nyumba yako ni ndogo kiasi gani?

blogger templates
Hapa ni sitting room, naomba niseme kitu kimoja, baadhi yetu, tumekua na fikra kua tukiweka fanicha za gharama ndio nyumba inapendeza....... ama tukijaza vitu kwenye nyumba zetu ndio kunapendeza,,..... tena hatuangalii ukubwa wa nyumba, chumba etc... ilimradi tuuu tuonekane nyumba imejaa ndio unajua kuko sawa.......napenda kuwaambia kua hapana.... hatuendi namna hiyo......
Nyumba hii ndogo, na anaekaa humu ameona ni bora aweke vitu vichache na vyenye sehemu ya kuhifadhi vitu..... kama hili kochi linavyoonekana, chini ameweka droo na amehifadhi vitu..... sasa kwa wewee mwenye nyumba ndogo, jitahidi ununue makochi ambayo yana uvungu, ili ule uvungu uweze kutumia kwa kuhifahdi vitu, unakumbuka vile vikapu nilivyo waonyesha? sasa angalia ukubwa wa kochi lako na uweke kama vitaingia 2 ama vitatu, na kumbuka kusafisha mara kwa mara ili kuepusha uchafu na uvundo.

kwa upande wa kitanda napo ni hivyo hivyo, tumia uvungu kuhifadhi kama ni nguo,, mashuka etc. na ukumbuke kufanya usafi mara kwa mara na kuepusha uvundo.... sio lazima kutengeneza kitanda kama hiki, hata ulichonacho kama kina uvungu, basi weka vile vikapu, ila ndio usivijaze huko uvunguni, maana utakua ni uchafu, 2-3 vinatosha.....
Jiko, hili dogo linatosha kabisa, kwa nyumba ndogo... na hapo hapo pakawa ni sehemu ya kulia chakula. weka jiko lako katika hali ya usafi wakati woote.... maana kumbuka jiko dogo, sasa likiwa haliangaliwi vizuri hali itabadilika na nyumba itazidi kua ndogo, na panya na wadudu wengine ndio watakua wageni....
Haijalishi, kua unapokua na plazma tv, basi ni lazima ukanunue tv stand ya plazma special....... hata ya mbao ama chuma pia itafaa tena hizo ni imara sana...
Bafu hili ni dogo mno, ila limewekwa vizuri, na kumbuka kwenye nyumba ndogo rangi za ukutani inabidi ziwe ni ng'aavu......zinasaidia chumba/nyumba kuonekana kubwa
Kwa upande wa jiko, jitahidi kuwa na sehemu za kuhifadhi vitu vyako nyingi, na uhifidhi kwa usafi...


Kua na nyumba ndogo sio eti ndio uwe mchafu, ama huwezi kufanya usafi, na kupaacha tuuu. ukihidhi vitu vyako vizuri, na ukiwa na nafasi ya kuhifadhi basi kila kitu kitakua poa.....

0 Response to "Nyumba yako ni ndogo kiasi gani?"

Posting Komentar