Nimewagusaaa eheheee!!!!

blogger templates





Inafika pahala sasa tuambizane ukweli....., watanzania asilimia kubwa hatuna hela si ndio ehee, ila hao hao utawakuta wanavaa vizuri, tena vitu vya designers, kama ndio nguo, cheni, viatu (CL) ndio vimeingia maana navisikia tuuu, lace wig kuchangia sherehe kwa kiasi kikubwaa cha fedha etc.

Wanakokaa hapafai na ni aibu jamani, yaani unamkuta mtu nje mrembo kavalia huyoooo, gari zuri ila nenda home kwake, jamani, unaweza ukakataa lol...

Hivi kweli uki save hela yako hiyo ukasema sasa mwezi huu ama miezi miwili sinunui nguo wala viatu etc, natengeneza nyumba yangu, kama ni yakupanga ama ya kwako, utashindwaaaa kweli, ama ndio kupanga kuchagua....

Hebu tujirekebishe sasa, na tuanze kupenda nyumba zetu, maana maisha yetu yanategemea sana nyumba zetu, na ukiipendezesha nyumba yako, basi na hata safari usizozipangilia na mafoleni haya kumaliza mafuta ya gari, na uchovu hata kama unapanda basi, zitapungua na utakua unarudi home kwako moja kwa moja kwa amani, na utapumzika kwa amani.....


Ni hayo tuuu kwa leo.........TUBADILIKE, NA HILI LINAANZA NA WEWE, SIE WENGINE NI WATAZAMAJI TUUUUU UKIJIBANA KWA MUDA UNAWEZA KUPAMBA NYUMBA YAKO NA IKAWA NZURI TENA ZAIDI YA HIZI............



0 Response to "Nimewagusaaa eheheee!!!!"

Posting Komentar