Maandalizi ya Website yakiendelea......

blogger templates
Mambo ya mtandao, sasa hatutembei na files za catalogue, ni kitu cha ipad hapa......Thanks Lord naendelea kupiga hatua taratibu kwa juhudi zangu mwenyewe......I love my self




Huyu ndie aliyewezesha website yangu mpaka iko hewani, na yeye ndie atakua akihusika na maswala yote ya website, isiende kombo.........ni web designer......sio kwamba ninamsifu, ila katika kutafuta web designer wa kunifanyia kazi yangu hii, nikakutana nae, tena nilimpata kwa mteja wangu mmoja ndio akaniunganisha nae. Anaitwa Kaduma huyu web designer wangu.

Yaani this guy, anajua anachokifanya, na anajua kazi yake, hana haraka haraka ya kufanya kazi bora liende tuu... ana anafanya kazi kulingana na wewe unachokitaka na anakupa ushauri, na hakatai mawazo. Na imetuchukua kama miezi 2-3 hivi, maana tulikua tukiiandaa na kupumzika na kutafuta hela... hhahha si unajua tena tunajikongoja... hahaa.... lakini hakuchoka wala kukasirika. etc..... kwa ufupi he is a great guy of all.......atakaemhitaji contacts zake ziko hapo juu kwenye tangazo.......then utakuja kuniambia.....


hahahaha, imetokea wote leo tumevaa blue..... hhahahaha.... ila tumependeza ehehehhe hahahaah

Bado tunaendelea na kuijazia sehemu ambazo zinahitajikaa, maana ninataka iwe ni directory ya Interior decorations, etc...... sasa jamani si kazi ndogo hii naomba tuwe tunavumiliana pale ambapo ninachelewa ku post, ingawa sitakua ninakaa muda sana..... na hii ni kwa ajili yenu ndugu watanzania wenzangu, ninataka ifike mahala sasa, unahitaji kitu basi wewe unaingia kwenye website na blog yangu na kutafuta kampuni unazozitaka, na kwenda kwenye website zao.... na hii naona itasaidia sana sana, wawe wana update website zao mara kwa mara kwa kuweka vitu vipya walivyoagiza.

Natumai kwa kufanya hivi jamani tutakua tunaokoa muda, maana kwa sasa unahitaji kitu nahujui wapi pa kukipata, mwishowe hela unakula.......

Kwa kusema ukweli hii kazi ni ngumu, maana ni mpaka makampuni yaelewe na wanikubalie, sasa sio kazi ya leo ama kesho kukubaliwa, ila ninaamini nikiianza mapema itakua rahisi kwetu wote sote...

Ninajaribu kuwapa mawazo yangu ya nini nafikiria kukifanya na wapi tunakwenda, ninahitaji ushirikiano wenu wa hali na mali, kwa kunivumilia ili tufikie malengo.....ifike pahala na sie tunaweza kununua vitu online kwenye makampuni yetu ya nchi yetu hii.......najua inawezekana na ndio maana ninataka kuifanyia kazi......

Jamani kuna watu wamekaa tuu na kutafuta mawazo ya watu na wao waige ili watoke....... naomba kusema kua sitoogopa, wala kumuonea mtu huruma, nikiona mtu kaiga haya mawazo yangu na kuyafanyia kazi........yaani nitamuaibisha mpaka atashangaaaa, na nadhani kwa hili ndugu wadau tutasadiana na watu wa namna hiiiii.

Kwa haya mafupi napenda kuwashukuru wote kwa kuendelea kua nami na mnaendelea kua nami maana bila ninyi nisingefika hapa nilipo na kujivunia kazi yangu......naendelea kuomba mawazo yenu juu ya hi website yetu, kama kuna kitu tuongeze, tupunguze, etc.... nitayapokea na kuyafanyia kazi....

Nawatakia weekend njema.......



0 Response to "Maandalizi ya Website yakiendelea......"

Posting Komentar