Mbezi Beach Project.....Iron furniture by Homez Deco.....

blogger templates
Asikuambie mtu fanicha za chuma zinapendeza sana... na hautogombana na dada wa kazi kua hafanyi usafi chini ya makochi......kote kunaonekana.....

Dinning table.......ya viti 5.....
Mto ukiwa na cusion cover na tayari kwenda kwa mteja...
Mto ukiwa na linning....
Kiti kikianza kuonyesha muelekeo....


Ninashukuru mungu kua sasa nimeweza kuwapatia vijana ajira hapa mtaani kwetu kwenye ofisi yangu........

Hapa nikikagua kazi, mito kama ujazo uko sawa na inakaaje kwenye kiti....kazi hazitoki mpaka nimezikagua.....


Hii ndio kazi ya yale magodoro madogo madogo ambayo tuliyakata kata vipande vidogo vidogo, tukavichanganya na fiber, na tukashona decron tunazitumbukiza ndani mchanganyiko huo, na tunashonea lining, mwisho tunashonea foronya ama cover, na mto unakua tayari.

Kama kawaida yetu Homez Deco, hatufichi kitu, mito yetu ni imara na haina harufu hata ukimwagia maji, utauanika na utakauka na hakuna harufu itakayotoka ama kutoa alama kwenye mto....maana tunaweka vitu visafi tuuu..... mito ni soft na inadumu kwa muda mrefu bila kusinyaa.....

Hii ndio ile nyumba ambayo nilitengeneza curtain poles za chuma, vitanda vya chuma, vya four posters, nikawaonyesha, na last week tukamaliza na meza ya chakula na makochi..... wishing you all the best my dear customers.......

Asante sana mteja wangu na zawadi yako ya magazine rack iko jikoni......nitawaonyesha......


0 Response to "Mbezi Beach Project.....Iron furniture by Homez Deco....."

Posting Komentar