HOMEZ DECO INAWATAKIA MAANDALIZI MEMA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN.....

blogger templates
 Siku ya tarehe 30/06/2013 ambayo ni jana, kulikua na mkutano wa wanawake wa kiislam, na pia kulikua na maonesho ya biashara, tunashukuru Mungu nasi Homez Deco tuliweza kuwepo katika hili, na tukauza pia baadhi ya vitu, na mimi binafsi nilipata mawili matatu, katika mawaidha......

Mimi Sylvia Namoyo, baba yetu alikua ni Muislam, na mama alikua ni Mkristo, nimetumia wakati uliopita, maana wazazi wote wako mbele ya haki, na Mungu amewapenda zaidi.

Nimelelewa katika malezi ya ukristo na mama mdogo......maana tuliachwa tukiwa wadogo.....mimi ni mtoto wa 4 wa marehemu Said Namoyo.

Kwa kweli ninamshukuru sana sana sana, mama yangu mdogo, ambae kwa kipindi hichi chote amenilea, na kunisomesha, na kuchukulia kama mtoto wake wa kumzaa mwenyewe, sijawahi pata mateso yoyote yale.
Mama yangu huyu anastahili pongezi sana sana, maana yeye ndie alienipa ujasiri na anaendelea kunipa ujasiri mpaka hii leo, nina biashara yangu, maisha yangu, mtoto wangu. na vyote hivi navimudu mimi mwenyewe.

Malezi aliyonipa mama yangu, ni yale ya kujitegemea mwenyewe, na si kutegemea cha ndugu ama mtu. Nikiwa nacho nashukuru Mungu, nisipokua nacho pia nashukuru Mungu, na ninaendelea kuongeza bidiiii....

Amenifunza mengi nikiwa mdogo, ingawa saa ingine akili za utoto unaona kama vile mmmmmhh, leo mama kapitiliza, ila sasa najionea ukweli wake, kua asingefanya vile, ningeaibika hapa duniani, na ningekua ni mzigo kwa kweli.

Siku ya jana ndio mara yangu ya kwanza kuvaa ushungi, kama ninavyoonekana, hua ninafunika tuu kichwa ilimradi, lakini kufunga kama inavyotakiwa ilikua ni jana.....

Kwa sekunde kadhaa, nilimkumbuka baba.....katika vazi hili.....ila ndio hivyo....Mungu amempenda zaidi.

Nawaombea Mungu aendelee kuziweka roho zenu wazazi wangu peponi......Amin. Tunawakumbuka sana sana.


Namuombea Mungu pia mama yangu aendelee kumpigania na kumuombea maisha marefu hapa duniani, maana yeye ndio kimbilio langu kwa hapa duniani, mimi na Jaydan wangu......

NB:
Kwa wale wote wanaolea watoto wa ndugu zao, kaeni nao vizuri, watunzeni, wasomesheni, kama watoto wenu, maana hamjui siku za mbele atakua nani, na ukute yeye ndie atakae kuja kukusaidia baadae.


0 Response to "HOMEZ DECO INAWATAKIA MAANDALIZI MEMA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN....."

Posting Komentar