Je unaweza kutumia email kuhusiana na usafi wa nyumba zetu, Tutumie email sylvianamoyo@yahoo.com nasi tutairusha humu

blogger templates


Jana nilitembelewa na mdau wangu hapa ofisini kwetu, alikuja kujua suala la rangi ana nyumba yake anataka apake...so tukaongea akaona catalogue yetu ya rangi za dulux...na tukakubaliana anitumie kwa email nyumba niweze kuiona na kushauri ni rangi gani apake na nyumba iweze kupendeza..

Sasa akanikumbusha lile suala la glass niliyoletewa ikawa inanuka mende....alicheka sana, na akasema yaani umeweza kusema, kumwambia mwenyewe, nikamwambia ndio maana nisingesema ningekunywa na huo uchafu.....

Sasa tukaanza na stori za hapa na pale, akaniambia hivi jamani bado kuna watu wanatandika vitambaa kwenye makochi, hivi hii fashion si imekwisha jamani, maana ilikua ni zile enzi za mababu na mabibi zetu zama zile.....Nikamwambia ni kweli sasa hivi hii mambo ya kutandika vitambaa kwenye makochi ni kizamani ila bado tunaendelea kuelimishana......na hatimae najua iko siku watu tutaelewa na kuacha kabisaaaa...

Tukahamia kwenye swala la usafi wa nyumba....yaani hapa nilijichekea kweli, maana kwa kusema ukweli kuna tatizo...kwanza kwenye products zenyewe za usafi, na pili usafi wenyewe...utakuta mtu anafanya usafi wa nyumba yake, ila ukiangalia darini kuna buibui wametanda,.....sasa huo ni usafi kweli.....

Kwenye usafi unapaswa huanzia juu kuja chini, sasa tatizo sijui linakuaga wapi buibui zinasahaulika....ukija kwenye usafi wa chini ya makochi....na haya masofa yetu haya yanavyohifadhi panya....jamani jamani.....

Nilishakutana na sofa ambazo ndani kuna panya......yaani nilikwenda kwa client, kuangalia anataka abadilishiwe kitambaa sofa zake...na hua ninasemaga sio kila sofa inafaa, kubadilishwa, ama kufanyiwa marekebisho sasa hua ninakwenda kuangalia.....yaani jamani sasa sijui kuhusu panya nikakaa kwenye sofa baada ya kukaribishwa, tukaanza kuongea, sasa nikawa nasikia vitu vinatembea tembea....lol....

baada ya dk 3 panya huyo chini ya kochi katoka na kaingia kochi lingine....yaani acha tuuu...niliruka, maana na ujanja wangu wote panya naogopa....

Kama kawa, sikuvumilia, nikamwambia hivi unajua panya wanaletwa na uchafu ambao ndio unaowavutia....sasa haya makochi hata kabla sijaendelea kuangalia, ninakushauri uyatupe, maana tukisema turekebishe ni sawa na kununua lingine.....na utakapo leta lingine, hakikisha unatibu hili tatizo la panya, kuna dawa, na uzingatie usafi wa ndani kwako.....tukawa tumemaliza....

Matatizo kwenye nyumba kuhusu usafi ni mengi mnooo, hatutumii products nzuri za usafi, ama tuna rashia rashia tuu usafi, ama tunamwachia tuu dada afanye usafi, etc.....

Ninakaribisha kwa yeyeyote yule mwenye tips za usafi wa majumbani atutumie email ili tuweze kuelekezana humu humu kwenye blog yetu hii nami nitairusha na kusahuriana.....hakuna anaejua wote tunajifunza kupitia kwa mwingine......na kuwekana sawa

Email: sylvianamoyo@yahoo.com

0 Response to "Je unaweza kutumia email kuhusiana na usafi wa nyumba zetu, Tutumie email sylvianamoyo@yahoo.com nasi tutairusha humu"

Posting Komentar