Homez Deco inaomba mawazo yenu juu ya hili, Ili tuweze kusaidiana kutekeleza, kwa ufanisi, (Umoja ni nguvu, utengano ni ......)

blogger templates
Nimekua nikipata kazi, kwa wanaohitaji huduma yangu, nashukuru mungu wanaikubali na wanaipenda, na nimekua nikiona kua nyumba nyingi zinakua na vitu ambavyo hawatumii, e.g sofa's, carperts, vyombo, tv, computer, vitanda, (visiwe vimechakaa sana, yaani vimetoboka ama kupasuka) etc. Nikaanza nao wao kwa kuwauwauliza, kama ikitokea wavipunguze wataweza kuvitoa bure/ kugawa.... maana wao hawavitumii, wengi wao wakasema sawa hakuna shida.

Sasa basi nikaona  niilete hii mada kwenu ndugu wadau, ni hivi, nimekua nikifikiria sana kua tutawasaidiaje hawa ndugu zetu, watoto wetu yatima?

Hivyo mi niliona kua, kama una vitu ambavyo hauvitumii, tutapanga ndani ya mwezi mmoja, Homez Deco, na wadau wengine watakaojitokeza kusaidia,  maana litahitajika gari la kufuata vitu majumbani etc. sehemu ya kuhifadhi hivyo vitu. tutavikusanya vitu hivyo, mpaka siku itakayokua imechaguliwa.

Lakini sasa, vitu hivyo vitauzwa kwa watu wa hali ya chini, na bei itakua ni karibu na bure, na hela itakayopatikana, itanunua vifaa ambavyo vituo hivyo vya watoto yatima wamevihitaji, na tutawapelekea.

Kwa mtindo huu tutakua tumewasaidia watu wa makundi 2 kwa pamoja. Watu wa hali ya chini. na watoto yatima.

Hii itasaidia sana kupunguza vitu visivyohitajika majumbani mwetu, na nyumba kua safi, ila nguo hazitaingia katika kundi hili kwa sasa.

Nashukuru sana kwa kua nami.

NB: Tayari nimeongea na Khadija Mwanamboka na amekubali tutasaidiana kwa hili, wengine ni marafiki zangu wa karibu, na wateja wangu wote wamekubali kusaidiana nami. Nawashukuru sana sana.

Zoezi hili likifanyika vizuri, tutaanza na mikoani pia, yaani kila mkoa, utakua umesaidia, vituo hivi katika mkoa wake.

Thanks,

From
Sylvia...a.k.a mama Jaydan

0 Response to "Homez Deco inaomba mawazo yenu juu ya hili, Ili tuweze kusaidiana kutekeleza, kwa ufanisi, (Umoja ni nguvu, utengano ni ......)"

Posting Komentar