Strechmark za kwenye tumbo wakati wa ujauzito

blogger templates

Napenda ku share na wadau wangu habari njema, ni kwa wale wote ambao ni mother to be na ambao watakao teegemea kupata watoto.

Hizi streachmarks kwenye tumbo, nilikua ninazisikia tuuu, ila nakumbuka siku moja wakati niko kwenye first trimester, nilikwenda mlimani city kwenye maduka ya watoto nikiwa ninafanya window shopping.

Nikaingia duka la mummys, nikafanya window shopping yangu, na wadada wa duka hilo ni wakarimu na walinihudumia vizuri, kuna dada mmoja muhudumu wa duka hilo akaniambia dada naomba nikupe ushauri kuhusu kukabiliana na strechmark, ndio akaniambia kua mafuta ya mgando, yaani vaseline, baby care etc hua yanasaidia sana.

Cha kufanya, paka tumboni mafuta hayo mengi ya kutosha tokea mimba ikiwa changa kila siku mara baada ya kuoga. Inasaidia sana kupunguza kuwasha na kutotoa strechmark

Akanionyesha tumbo lake kweli halikua na strechmark yoyote, na mtoto wake that time alikua na miezi 4.

Kweeli nilichua ushauri wake na kuufanyia kazi mara moja. YAANI HAMUWEZI KUAMINI ILA NDIO HIVYO SINA STRECHMARK MPAKA SASA NA  NIKO SECOND TRIMESTER, NA KUWASHWA TUMBO NI MARA CHACHE. NINAMSHUKURU SASA YULE DADA KWA KUNISAIDIA (KWA KWELI KAMA NINGEWEZA KUWAONYESHA TUMBO LANGU NINGEWAONYESHA MJIONEE ILA UTAMADUNI HAURUHUSU KWA KWELI)


0 Response to "Strechmark za kwenye tumbo wakati wa ujauzito"

Posting Komentar