Ubatizo wa Jaydan, ilikua ni tarehe 1/9/2012

blogger templates
 Jaydan akiingia kanisani na dada yake
 Tuko kanisani tayari na Jossyanne ndie mama wa ubatizo wa Jaydan

 Jaydan akibatizwa akiwa ameshikwa na mama yake wa ubatizo.....kwa kweli machozi yalinilenga lenga kwa furaha.......
 Kwa sisi wa kristo tunakua na kitu kimoja kwamba ukizaa nje ya ndoa basi unatengwa, sasa unahitajika kurudi kanisani na utubu dhambi zako, na hapa ndicho kilichokua kikifanyika.....

 Nilipewa mtoto wangu baada ya kurudishwa kanisani, na tuliombewa.... yaani nilijihisi nimetua mzigo maana kifua kilibaki chepesi sna..... namshukuru mungu kwa kila jambo analonitendea na mwanangu.....mungu ni mwema
 Jaydan baada ya kubatizwa......nakupenda sana mwanangu kuliko kitu chochote hapa duniani....tuna mwaka na miez sita sasa....
 familia... akiwa na bibi na shangazi
 Hapa Jaydan akiwa na bibi yake mzaa mama  na mama yake...
 Jaydan na mama wa ubatizo na mie nina mtoto wa ubatizo jina lake ni Samantha ana miezi 5....nina watoto 2 sasa... nawapenda wote
 Tukiwa na mtoto wetu wa ubatizo Samantha, huyu ni kaka yangu.....
 Jaydan na bibi na mama
 Haya huyu ndie baba wa ubatizo wa Jaydan ni mdogo wangu
 Na huyu ndie mama wa ubatizo Jossyanne. wengi wenu mwamjua....love u sis....n anakushukuru kwa kua nasi siku hiii....
 Mama mzaa chema.... hahahhaha
 Jaydan katika pozi.....
 Kwa kweli nina kila sababu ya kumshukuru dada anaekaa na Jaydan, maana sijui ingekuaje, kwa kazi ninazozifanya narudi usiku, nimechoka, na namkuta Jaydan hana tatizo lolote kwa kweli. nakushukuru dada Jaydan. Ninae tokea nimejifungua Jaydan....
Familia baada ya kutoka kanisani...... nawapenda wote.....

NB:
Ubatizo ulikua wa kimya kimya jamani samahani sana kwa kua mchoyo kuwakaribisha.....nawapenda wadau wangu woteee

0 Response to "Ubatizo wa Jaydan, ilikua ni tarehe 1/9/2012"

Posting Komentar