Nikiwa najiandaa kuanza kutengenezwa......
Nikitengenezwa.........
Kucha zangu tayari sasa........
Her name is Rahma- Owner of Candra Saloon - 0712 - 007077
Candra saloon iko kinondoni, pembeni na barclays bank kuna ghorofa, saloon hii iko hapo...... Ninachokipenda kwa sasa asilimia kubwa ya sisi wanawake tuko juu tunajishughulisha kwa kufanya kazi na biashara, hatuna uoga kama zamani, ama tunasubiria tuuu tuletewe hela....
Saloon hii kinachonifurahisha ni usafi, na huduma zake..... nimependa pia mwenye saloon alivyoweza kupamba saloon yake, na kutumia space vizuri, kwani kabla ya kufanya kitu, ni lazima ujue ukubwa wa sehemu yako, na nini uweke na nini usiweke...
Hauhitaji kua na space kubwa, ndio biashara ionekane, kila mtu anafanya biashara kulingana na uwezo, sasa kwa baadhi, ya watu bado wana ile dhana kua, mpaka kitu kiwe kizuri ni mpaka pawe pakubwa, ama barabarani etc.......
Kinachohitajika ni huduma nzuri, kazi iwe ni nzuri. etc. ukiwa na hivi vyote, basi kokote uliko utafikiwa, tusiogope kufungua biashara eti nani atasema nini ama atasema vipi.........
Hii ndio saloon wananitengeneza kucha zangu, kwa kweli mwanzoni nilikua sina mawazo ya kucha..... lakini walinifanya nimeanza kupenda kucha zangu na kutengeneza.
Service zao ni nzuri, kingine ni kwamba, ukiwa unataka kupaka rangi ya miguuni, basi wanakusafisha kwanza. sio kama baadhi ya saloon zingine, hua wanakufuta, tuu rangi halafu wanakupaka, hapa wanakuosha ndio wakupake,.....
Na pia ukipenda wawe wanakukumbusha appointment yako ya kucha wanafanya hivyo...
Karibuni sana sana.... na bei zao ni nzuri tuuuuu.....
0 Response to "Introducing Candra Saloon.........(Wanawake tuko juu sasa.......)"
Posting Komentar