3d ni michoro ambayo huchorwa kwa kutumia computer na software maalum, ili kuweza kuona ni jinsi gani jengo lako itakua tayari baada ya kujengwa, na muonekano wake kwa ujumla, mpangilio wa fanicha ndani, na kuweza kukuonyesha makosa madogo na makubwa......
Hapa chini ni baadhi ya michoro ya 3d, ambapo tumeweza kuonyesha mfano wa nyumba itakavyoonekana baada ya kwisha kujengwa kwa nje....
3d yaweza kua niya garden, ya nyumba nje, ya mpangilio ndani, etc....ni wewe mwenyewe unahitaji nini.....
Kitu kingine nimegundua kua katika ujenzi wa nyumba zetu, hua hatuna ule utaratibu wa kua wawazi kwa archtects(wachora ramani). Hausemi nini unataka, yaani we umeona nyumba ya flan basi unataka kua kama na yake na inabadilishwa kidogo tuuuu.......(copy and paste).
Jamni designs za nyumba ziko nyingi mno.....na ndio maana utakuta hapa kwetu nyumba zinafanana mno.......ukiona nyumba imebadilika basi ujue hiyo nyumba mwenye hakai sana hapa, kaja na mchoro wake toka nje.....
(nitalizungumzia hili siku ingine kwenye mada yake) inafika kipindi tuambizane ukweli....sasa......(let's be creative)
kwa upande wa 3d, kama tungekua tunafuatilia ama kujua mapema, wengi wetu tusingekumbana na matatizo haya....maana saa ingine utakuta ukuta umezidi, inabidi kubomoa.......sasa hizo ni gharama zisizokua na maana.......
3d inakusaidia kukuonyesha ni jinsi gani nyumba yako itakavyokua imekwisha na kwa muonekano gani....na sio tuu kwa nje, hata kwa ndani ya nyumba yako ama ofisi yako, utumie rangi gani, fanicha za aina gani, zikaeje, mapambo pia yaweje na yakaaje......
kwa mpango huu yaani haya makosa hayatakuwepo kabisaaaa
Kuna wengine utakuta kiwanja ni kidogo nyumba ni kubwa....na hii hutokana na kwamba wengi wetu hatujui vipimo vinavyoandikwa kwenye ramani.......so ukiona tuu vile vipimo unajua nyumba ni ya kawaida,,,,,ama kiwanja kikubwa nyumba ni ndogo.......ama nyumba imekaa pembeni ya kiwanja, ama mbele unaacha nafasi kubwa nyuma, ama nyumba imegeuka.........wengine wananiambia unajua nyumba ya kwanza lazima kunakua na mapungufu, so tunajifunza kupitia hii ya kwanza.....itakayofuata tutakua tumeshajifunza....
Jamani, hakuna kitu kama hicho, ukitumia mtaalaam, tena mwenye kupenda kazi yake, kwa moyo wake wote na asiye na tamaaa.........Maana katika ku design 3d, jamani, kwanza akili iwe imetulia, na inahitaji muda wa kutosha, hakuna kitu kinaitwa haraka haraka.....kumbuka unatumia hela kujenga, na ukijenga umejenga......mambo ya kubomoa haifai na haipendezi..........
Yote haya niliyoyataja, ndugu wadau wangu ninakutana nayo mnooooooo, na ukiuliza kwanini imekua hivi, jibu ninalolipata ni kua wengi hawajui vipimo, na hawachorewi 3d kuona nyumba inakuaje ikishamalizika........
Homez Deco, tunapenda kuwakaribisha wadau, wateja, marafiki, ndugu, na wote, kua tumeanzisha huduma ya kuchorewa 3d.....na hii itakusaidia sana kuepuka gharama zisizohitajika wakati utakapoanza ujenzi wa nyumba yako ama ofisi yako........
Tutaendelea kuwaletea na kuwaelimisha kuhusu 3d designs, na nawaomba msisite kutupigia simu: 0713 - 920565 ama kutuandikia email: sylvianamoyo@yahoo.com
0 Response to "3D DESIGNS......"
Posting Komentar