Nimekua kimya kiasi, ila ni kutokana kuna habari nzuri nitawaambia humu humu.....hivi karibuni, maana haukua ukimya wa bure....
Haya turudi kwenye mada.....Siku hizi katika nyumba nyingi ambazo ninazifanyia kazi asilimia kubwa ya nyumba hizi kuna chumba wamekitenga kwa ajili ya ofisi......na ukubwa wa vyumba hivi vinatofautiana, hivyo nimeonelea nilete angalau design mbili tatu watu waweze kujua ni nini uweke, ama nini ufanye ama kama ulikua hauna lengo la kuweka basi upate hata wazo....
Ofisi za majumbani, hazihitaji vitu vingi, ama marembo mengi....jitahidi ziwe simple na ya kuvutia, na pamba ofisi yako kulingana na ukubwa wa chumba chenyewe....
Weka fanicha za kutoshea chumba, na hakikisha kuwe na nafasi ya kutosha umeiacha, na mwanga na hewa uwe unaingia wa kutosha, kuepuka uvundo.....
Rangi pia ziwe ni angavu na za kuvutia.....kwenye chumba hiki tusipende kuweka rangi za kiza...maana kutakua kuna kusoma, kuandika etc......rangi ang'aavu zitakusaidia kuona na kufanya kazi zako vizuri......
Taa pia iwe ya kutosha kuongeza mwanga....
0 Response to "Ofisi za majumbani..."
Posting Komentar