Hiki ni chumba cha 8 kwa 10, sio chumba lazima kiwe kibwa ndio uwe na walk in closet, mpangilio huu, husaidia sana kukuweka msafi wa nguo zako, na kujua ni nguo gani niitoe/kugawa kabla ya kununua nguo ingine.
Pls, jitahidi kabla ya kufanya shopping ya nguo, angalia kwanza kabati lako ni vitu gani utoe ili kupunguza msongamano na mlundikano wa vitu kabatini, zoezi hili ni rahisi, maana kama tunaweza kuandika list ya vitu vilivyoisha jikoni ndio tukanunue, sidhani kama hii itashindikana, na itakusaidia kufanya budget, na kuto nunua vitu ambavyo huitaji.
Design hii ya kabati siwezi kusema ni rahisi, maana mbao zinapanda bei kila kukicha, na siku zote cheap is expensive.
Watanzania asilimia kubwa tunaogopa gharama tukidhani kua tunakua tumeokoa fedha zetu, kumbe ni gharama mara mbili mpaka tatu. Ni bora ufanye kitu kimoja kizuri kwa mara moja.
Kam nilivyosema, kila kitu kinachoonekana hapo kipo hapa kwetu Tanzania, na inawezekana.
Tuwasiliane kwa mahitaji ya closets za kisasa za mbao zetu za tanzania.
0 Response to "WALK IN CLOSET"
Posting Komentar