Hapo juu ndivyo palivyokua baada ya heka heka kupaandaaa. kwa wale waliofanikiwa kwenda saba saba ya mwaka huu, hii ni kazi ya homez deco. Tuli design, na kushona kuanzia pazia, bedcover, foronya za mito, scarting ya kitanda. Theme ilikua ni honey mooners room kwa upande wa hotel.
Baada ya heka heka, na wateja wangu walifurahi kazi yangu, kitu ambacho ni muhimu katika kampuni yangu. maana ninaweza nikakosa usingizi, mteja anapokua hakuridhika...( si unajua customer care tenaaaa, niliyofundishwa na chuo hikiiii, )
Hapa ni katika hatua za mwisho za kukagua kazi tuliyoifanya, je inaridhishaaaa!!!! (guess what, huyu ndie bibi yake Jaydan) ni tutor wa chuo cha taifa cha utaliii, upande wa rooms division... Love you mama.....
Huu ni mfano wa jiko la hotel
Na hili ni trolley la housekeeping, hotels zote ni lazima hili trolley liwepo, lina rahisisha kazi kwani linabeba kila kitu kinachohitajika na usafi...( kweli hiki chuo cha taifa wamejipanga , yaani ukimaliza course yako, kazi nje nje) Like me nilipata kazi Golden Tulip, tena hii ilikua baadaya ya kumaliza field, wakaniita. Mungu ashukuriwe...
Tusishangae visu, kila kimoja kina kazi yake hapooooo, na hizo pombe ni mfano wa bar
I loved this table cloth color, hapo ni restaurant.
Yaani hapo ni bussy kweli kweli
NB:
Nilikua kimya but kazi zilikua zikiendelea kama kawa, so msishangae ninawaletea vitu vya miez ya nyuma, mniwie radhi.......
0 Response to "Saba Saba 2011 (Banda la Maliasili, upande wa chuo cha taifa)"
Posting Komentar