Mwaka huu wadau wa blog hii wameamua.......Wale wote walio kwenye kundi la 1, tunawashukuru, na kundi la 2 tujitahidi kufikia kundi 1......Kupanga kuchagua....Homez Deco tuko kwa ajili yako.....

blogger templates
Kundi la 1:

Tokea mwaka jana mwishoni mpaka sasa, kwa kweli napenda kuwapongeza wadau wangu kwa uamuzi wenu, kwa kuchagua Homez Deco, kuwafanyia kazi zenu.

Yaani naanza kuona matunda ya kile ninachokifundisha....... kama ninavyosema, Kupanga kuchagua. Ukichagua kuvaa, ukaacha nyumba haieleweki ni umechagua, na ukichagua kutengeneza nyumba mambo mengine baadae pia ni kuchagua.

Uamuzi ni wako, chaguo ni lako.

Tumepata pongezi nyingi sana sana, kwa wateja wetu wote tuliowafanyia kazi, maana kwanza tuna meet deadline ya delivery, kazi ni nzuri....... hakuna longolongo, nawashukuru sana.

Kitu kingine ninachokisisitiza, na kimeshaanza kuleta matunda kwa wale wanaokitumia ni kwamba, ku decorate nyumba yako sio lazima ufanye vitu vyote kwa wakati mmoja,

 Kundi La 2:

Kua na check list ya nini kianze na nini kimalizike. Kwa kufanya hivyo utaona utakavyofanikiwa, na budget yako haitaingiliana na kitu kingine....

Hivi kama tunaweza kujiandaaa miezi na miezi kuchangia kitchen party, sendoff, harusi, na tena siku hizi sherehe zi nazidi, kwa nini tunashindwa kujipanga kukarabati nyumba zetu?

Najua ni gharama, ila ukijipanga inawezekana, na utaweza...... Inaanzia kwako na si kwa jirani.....

Chagua unaanza na chumba gani? na unamalizia wapi?

Kuna huu msemo hua ninakutana nao kila kukicha........SIWEZI DECORATE NYUMBA YA KUPANGA MPAKA KWENYE NYUMBA YANGU....

Sasa ukiliangalia huu msemo kwa mapana jamani, unajua inachekesha, maana emagine huyu mtu hana hata kiwanja.......ama ana kiwanja hajaanza kujenga, na hajajua ataanza lini kujenga.  Ila anavaa vizuri kupita maelezo, SASA KWA NINI UVAE VIZURI WAKATI UKO KWENYE YAKUPANGA, SI USUBIRI UWE NA YAKO NDIO UVAE VIZURI....(kwa mimi huu msemo ninautafsiri kua nyumba za kupanga haziihitaji decorations. hivyo hata kuvaa pia hakutakiwi kuvaa vizuri ukapendeza mpaka kwenye nyumba yako)

Ukiangalia kwa undani, unaweza decorate kwenye hiyo nyumba yako ya kupanga, na asilimia kubwa ya decorations ukaondoka nazo kwenye hiyo nyumba yako utakayojenga.

Naomba huu msemo wapendwa watanzania tuufute...... na ufutike..........

Nyumba nzuri inaanza na wewe na si mwenyenyumba, ama jirani........jipange, tayarisha checklist yako, na utaweza..... mungu ni mwema na anampa kheri yake kila mwenye nia....

Uko kwenye kundi gani?

Nawatakia siku njema.......

0 Response to "Mwaka huu wadau wa blog hii wameamua.......Wale wote walio kwenye kundi la 1, tunawashukuru, na kundi la 2 tujitahidi kufikia kundi 1......Kupanga kuchagua....Homez Deco tuko kwa ajili yako....."

Posting Komentar