Haya, hii ndivyo ilivyokua kwenye interview na capital radio leo......

blogger templates


Interview ilikuanza saa sita mchana, na nilihojiwa na Sara, ilikua ni kuhusu kupamba living room yenye space ndogo, so maelezo yakawa kama yafuatavyo....

Katika kupamba living room yenye space ndogo, kwenye upande wa rangi inatakiwa tupake rangi, zilizoko kwenye group ya cool colors, ambazo ni Blue, green, violet ziwe light. rangi hizi zinafanya chumba kidogo kua kikubwa,

Kwa upande wa fanicha, hapa inabidi tuweke fanicha ambazo ni mult purpose, nikiwa na maana kua kama ni tv shelf, liwe linaweza kuweka magazine, tv, vyombo kiasi etc, ukija kwenye sofa ni L-shape pekee ndio itakayopendeza hapo, stools zile za sets, yaani zinakua zinaingiliana, kama mnazijua zinakuaga ni 3 size tofauti.   

Carpet, unaweza kuweka wall to wall carpet, ama kama kuna tiles, basi weka carpet za round, ama pembe nne etc, ziwe ni ndogo.

Tukamalizia na mapambo, kua weka picha za ukutani za wastani, kama ni 1, ama kama ziko tatu basi zipange vizuri zikifuatana.

NB: kuna kitu tunakiita Focal point kwenye interior design & landscaping, maana yake ni kua, ni kitu chochote kinacho attract macho cha kwanza kukiona uingiapo mahali. sasa yaweza kua ni garden, picha za ukutani, pazia, sofa, music system etc.

Nawashukuru sana Sara na Hawa wa Capital Radio kwa kunipa chance hii ya kuongea na watanzania wenzangu na kuwaelekeza nini cha kufanya na living room zao........

Na hapo ndipo tulipoishia,..... nitawajulisha ni lini tena tutaendelea na mafunzo haya.........Capital Radio......

0 Response to "Haya, hii ndivyo ilivyokua kwenye interview na capital radio leo......"

Posting Komentar