Nyufa kwenye ukuta wa makazi yetu

blogger templates

Nimepata experience ya kua nyumba nyingi kabla hata ya mwaka zinakua zina ufa, eidha ni kuanzia chini ama juu.

Hii ni kutokana na kua mafundi wengi tunawaowachukua watujengee wamekua ni waongo ama tunataka cheap labour, ama tunaowapa wasimamie nyumba zetu wamekua wakila hela, wachora ramani feki etc. sababu ziko nyingi.

Sasa basi sio watu wote wana muda wa kusimamia nyumba zao wakati zinajengwa, na hii  ni kutokana na kwamba hali ya maisha imekua ngumu siku hadi siku.

Tumekuwa tukiharibiwa nyumba zetu na kuliwa hela pasipo na sababu za msingi.

Nimejaribu kutafuta ushauri kwa wataalam wa mambo haya, ambao ni archtect etc.

Wamenipa ushauri na kama kawaida hua nina share nanyi ninapopata mambo mazuri.

  1. Jitahidi kupata ushauri kwa wataalam, kama contractors, artchects etc. ambao wamesomea na hiyo ndio fani zao.
  2. Acha kuchukua cheap labour.
  3. Kama una uwezo wa kifedha ni bora ukamtafuta contractor akakujengea nyumba yako, hii inasaidia kua kama kutatokea tatizo lolote lile yeye ndie atakuwa responsible, najua ni gharama, lakini ni afadhali nusu shari kuliko shari nzima.
  4. Kua makini na mafundi maana sio kila fundi ni fundi, kama hutoweza kuchukua contractors maana unaweza ukachukua dalali, ama msaidizi wa fundi akakuambia yeye ni fundi kumbe sio fundi. Utapeli ni mwingi sasa.

Kwa kweli sababu ziko nyingi sana, na nitaendelea kuwaletea ushauri, na sasa niko kwenye mchakato wa kuwatafutia contacts zao ili, muwasiliane na wawape ushauri pia.

NB: KUA MAKINI MATAPELI WAKO WENGI SASA, NA SIO KILA MTU AKIKUAMBIA YEYE NI FUNDI BASI UKAMUAMINI, GHARAMA YA KUREKEBISHA MAKOSA NI KUBWA ZAIDI YA UNAVYOFIKIRIA.

0 Response to "Nyufa kwenye ukuta wa makazi yetu"

Posting Komentar