Rabu, 31 Oktober 2012

Before It's Too Late!

Happy Halloween, everyone!  Can you believe it's already here?  I canNOT!
 
If you saw my house right now, you'd laugh because it's suffering a serious identity crisis!  The outside is decorated for Halloween ... the kitchen has the beginnings of Christmas ... and, the sitting room has Fall splashed around.  I almost feel sorry for it (and, me, lol)!
 
Before the leaves and pumpkins are put back into the Fall bins for another year, I snapped a few pics of our sitting room, dressed in blues, creams and pops of vibrant orange.
 
 

Glass cloches are often my BFF when it comes to styling ... they're the perfect way to showcase ANYthing, aren't they?


When I spotted "Mr. Owl" at Michael's, I just *knew* he had to come home with me ... esPECIALLY since he was on sale (40% off)!

 
Once again ... another glass cloche to the rescue.

 
 
I still can't wait to change out our chandelier!



Behind the loveseat, I added a sofa table recently picked up from a consignment shop.  You know I love having another place to add a few goodies:

 

More pieces of orange found its way to our accent chest, too. 

 
 
My favorite part of the day is when the afternoon sun shines in:
 
 
So, tell me ... is your house suffering an identity crisis right now, too?
 
I'm joinging:
 
Savvy Southern Style/WUW
Kristen's Creations/Share Your Creations
French Country Cottage/Feathered Nest Friday
At the Picket Fence/Inspiration Friday


 

post signature

Usafi wa majumbani kwetu.....



Tumekua tukiongelea sana kuhusu kupamba nyumba zetu, na kuzipendezesha......sasa vipi kuhusu usafi? Je usafi wa nyumba yako uanzingatia? Kuanzia usafi wa vitendea kazi, sabuni uzitumiazo. zinakusaidia ama kukurahisishia? kwa wale wenye carpets, tiles, sofa za leather, sofa za vitambaa, etc......Unafanyaje usafi?

Majibu ya maswali haya utayapata humu humu....endelea kua nazi......

Je ungependa chumba chako kiwe na mandhali hoteli za kimataifa?







Kuna msemo usemao kupanga ni kuchagua........Sasa je, ungependa chumba chako kiwe na mandhali ya hoteli ya kimataifa?

Unachotakiwa kufanya ni.
 kwanza, chumba chako kipigwe rangi vizuri, na kiwe kisafi juu mpaka chini. Rangi waweza piga kama ni nyeupe ama rangi zilizopoa...

Pili, kama chumba chako hakina tiles. basi weka carpet chumba kizima, na kama kina tiles basi weka carpet ndogo, 

Tatu, weka pazia nzuri pamoja na curtain poles, ama curtain box... na hakikisha pazia zako zimeacha inch 2 ama 3 toka ardhini......nikiwa na maana zisiburuze.

Nne, kitanda ulichonacho ama kama ungependa kubadilisa, hamna neno,  hakikisha tuu gororo lako ni zuri nani kubwa nikiwa na maana lina inch 8 upana...maana hii husaidia kua na muonekano mzuri ukitandika....na haijalishi ni kitanda cha mbao ama cha chuma, vyote hupendezaaa...bila kusahau kuweka picha juu ya kitanda upande unaolaza kichwa

Tano, Tukija kwenye mashuka, sasa hapa shuka zinazohitajika ni zile zenye duvet, nikisema duvet ninamaanisha ni ile mfano wa godoro lakini lenyewe ni laini sana, maana wanaweka fibre ndani.....hapa kwetu yako madukani, kama Home shopping center, Mr. price etc...

Sita, ukija kwenye utandikaji sasa, unatakiwa uwe na shuka la kutandika, shuka la kujifunikia, halafu duvet ambalo ndio limevalishwa cover ya shuka la mwisho.....

Saba, tunakuja kupande wa mito, mito waweza kuanzia mito 4,5,6 ni wewe tuu unapenda kua na mito mingapi kitandani kwako, na kumbuku hii inakua ni set nzima......

Nane, kuna kitambaa kinaitwa scarting, hiki ni kitambaa ndio kinaanza kabla ya godoro ili kuficha uvunguni.....na kinakaa katika vitanda design yoyote ile..

Tisa, throw ama bed runner, hua ni kitambaa cha urembo ambacho hutandikwa kwa upande wa miguuni kwa upana....

Kumi, unahitajika kua na stools za pembeni mwa kitanda, sasa hizi zinaweza kua ni 2 ama moja maana inategemea na ukubwa wa chumba chako....juu ya hizo stools unahitajika kuweka taa, taa hizi ni ndogo na ni za urembo pia na husaidia pia kwa wale wanapenda kusoma, ama ambao hawapendi mwanga mwingi.....

Mwisho, ndio unakuja kwa upande wa dressing table, na kabati la nguo........

Hakikisha usijaze vitu sana chumbani, na ndio maana wengi wetu tukienda kwenye hotels tuna relax, hii ni kwa sababu wenzetu wana kua na mpangilio mzuri sana, na wanazingatia usafi kila siku iendayo kwa mungu.....


Ubunifu......

 Pazia hii ametumia ngozi ya mnyama kuweka urembo kama inavyooneka.....na imependeza.......kuiangalia pia kitandani kaweka ngozi ya mnyama kama bed throw......inapendeza kwa kweli....
Hapa sasa, badala ya kutumia shower curtain, pazia ndio imetumika......hapa usafi zaidi unahitajika.....maana shower curtain ni plastic, sasa hiki kitambaa cha pazia.......

Napenda kijani hii

Rangi hii ya kijani ni nzuri sana, na hufanya mahali ulipoipaka pawe pakubwa na kuvutia.... Kijani hii ni nzuri sana kwa sehemu zifuatazo, sebuleni, jikoni, kwenye korrido na hata kwenye sehemu za biashara....

Kumbuka waweza kuipaka ukuta mmoja, ama kuta zote, ama kuta mbili.......

Kwa vyumbani rangi hii sishauri sana kwani inawaka sana, na vyumbani hutakiwa rangi zilizopoa.....na kama unataka kupaka rangi kijani, basi tafuta iliyopoa zaidi.... hii inawaka sana.....

Senin, 29 Oktober 2012

Umejiandaaje kumaliza mwaka kwa upande wa nyumba yako?

Mwaka ndio huu unakaribia kuisha, na wengi wetu tunajitahidi kumalizia nyumba zetu, ili tuweze kuingia na kusherehekea tukiwa kwenye nyumba zetu....

Lakini pia kwa wale ambao bado, basi hata nanyi hamtakua nyuma kwa hili.(nikiwa na maana sio lazima uwe umejenga, hata kwenye nyumba ya kupanga unayookaa unaweza ukaipendezesha na ukasherehekea sikukuu vizuri tuu na familia)

Homez Deco inawakaribisha wote, kwa mahitaji yafuatayo:

1. Pazia
2.  Ushauri
3.Mpangilio wa fanicha
4.Rangi za ukuta, na ukizingatia tuko na rangi za Dulux za Sadolin
5. Thamani za chuma
6. Mapambo ya nyumba....

Muda ni mchache, tuwasiliane kwa maelezo zaidi.......0713-920565



Vitanda vya chuma...... karibu utoe oda.....vitanda ni bila godoro.. na usafiri ni juu ya mteja.....karibuni. (size zote zinapatikana kuanzia 3,4,5,6,& 7 by 6)

 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 380,000/-
 Size 5 by 6 395,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 380,000/-
 Size 5 by 6 395,000/-
 Size 5 by 6 380,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 380,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 380,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 380,000/-
 Size 5 by 6 350,000/-
 Size 5 by 6 380,000/-
Size 5 by 6 380,000/-

Uzuri wa sebule......





Angalia picha hizi na uone uzuri uko wapi wa hizi sebule. Je ni lazima uwe na fanicha za gharama ndio sebule iwe nzuri, ama ni mpaka vitu vijazane ndio sebule iwe nzuri. ama ni nini haswa hufanya sebule kua nzuri.....

Kwa muono wako wewe unaonaje?

Ukiniuliza mimi jibu ni kwamba, haijalishi eti mpaka uwe na fanicha za gharama, ama ujaze sebule. n.k. hapana. Sebule yako hiyo hiyo uliyo nayo, ukiibadilisha kwa kupunguza fanicha zilizojana ili uweze kupata nafasi, ama kuongeza vitu kidogo kwa sebule iliyo pwaya , ama kwa kubadilisha zulia lako kama limechakaa, badilisha kitambaa cha sofa pia kama kimechakaa (kama bado unalipenda sofa lako), bila kusahau rangi za ukuta pia, paka rangi kulingana na ukubwa wa sebule yako na fanicha zilizomo kumbuka rangi zenye giza hufanya chumba kuonekana kidogo, na zenye mwanga hufanya chumba kuonekana kikubwa......

Weka picha za ukutani, hapa haijalishi kama ni za familia ama urembo... ila tuu ziwe kwenye mpangilio mzuri na uwiano mzuri unaoendana....

Usafi wa mara kwa mara pia huhitajika.....

Bila kusahau upande wa pazia, mapambo kama mito, maua, taa, etc...

Hapa sasa utakua umepata muonekano mzuri  wa sebule yako........